GET /api/v0.1/hansard/entries/1037072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037072,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037072/?format=api",
    "text_counter": 440,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda. Mimi nawazungumzia watoto kule Kaunti ya Nyamira na Nairobi ambao wamezoea ile Kiswahili ya Sheng . Nataka kuwatia moyo kwamba Serikali imeweka mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba wakirudi shuleni mwaka ujao, hawatakuwa kwenye hatari ya kupata ule ugonjwa wa COVID-19. Nikimalizia kuhusu COVID-19, ningemuomba Rais wetu aangalie upya ile mikakati ambayo imewekwa kuthibiti huu ugonjwa wa COVID-19, haswa wakati huu ambapo tunaelekea katika ule msimu wa Krismasi. Kutakuwa na watu wengi ambao watakuwa wanakusanyika wakiwa katika sherehe za kuburudika na familia na marafiki. Bw. Spika wa Muda, lakini hatari yenye iko ni kwamba, wataki ambao watu wanakusanyika wakiwa wanafanya sherehe na kuwa katika sherehe za maankuli, huo ndio wakati ambao kuna hatari kubwa sana ya kusambaza huu ugonjwa wa COVID-19. Nataka niombe kwamba pia Rais atakaporejea tena Bungeni mwaka ujao, atueleze shughuli ambayo Serikali imefanya kupigana na janga la COVID-19. Ni vizuri kwamba, Serikali iangalie upya ile mikakati ambayo inaweza kuwekwa wakati huu wa msimu wa Krismasi. Hii ni ili tuweze kudhibiti zaidi huu ugonjwa wa COVID-19. Bw. Spika wa Muda, kumbuka kwamba mwaka ujao kutakuwa na wanafunzi wengi ambao watakuwa wanarejea shuleni wiki ya kwanza ya mwezi wa Januari mwaka wa 2021. Ni vyema tuweze kuzuia kueneza huu ugonjwa ili kuhakikisha kwamba, watoto ambao watakuwa wanaenda shule mwezi wa kwanza mwaka ujao, wasiende kama wamepata ugonjwa wa COVID-19. Bw. Spika wa Muda, hii ni kwa sababu itakuwa ni hatari sana kwa wanafunzi wengine kupata ugonjwa huu haswa walimu. Pia ni vizuri Serikali zetu za kaunti zihakikishe kwamba zimeweka mikakati ya kuwa na vitanda vya kutosha vya kulaza wagonjwa mahututi. Hii ni kwa sababu tukishamaliza huu msimu wa Krismasi, kuna hatari kwamba ugonjwa huu utapata tena mchangamko wa kuenea zaidi katika taifa lote. Pia namshukuru Rais kwa hiyo Hotuba ambayo alizungumza kuhusu maneno ya Building Bridges Initiative (BBI). Nia yake ni kuwaunganisha Wakenya na kuhakikisha kwamba sisi sote tunaenda mbele kama taifa. Bw. Spika wa Muda, ningependa kumshukuru sana kiongozi wa taifa pamoja na kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. Hii ni kwa sababu walihakikisha kwamba baada ya kupokea maoni kutoka kwa wananchi, ile ripoti ambayo tumeipata sasa ya BBI imeshughulikia mikakati ama mchangamko ambao Wakenya walikuwa wamezua kuhusiana na ile ripoti ya kwanza. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}