GET /api/v0.1/hansard/entries/1037073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037073,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037073/?format=api",
    "text_counter": 441,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "Nikizungumza kama Seneta wa Kaunti ya Nyamira, nataka niwashukuru sana. Hii ni kwa sababu tulipopata hii ripoti mara ya kwanza sisi hatukuwa tumeongezewa eneo Bunge katika kaunti yetu ya Nyamira. Lakini baada ya wengine wetu kuteta sana na kusema kwamba hatungekubali hii BBI kama hatungekuwa na eneo Bunge limeongezwa kule Kaunti ya Nyamira, nafurahi sana kusema kwamba sasa Kaunti yetu ya Nyamira imeongezewa eneo moja la Bunge. Ikiwa BBI itapita, sisi watu wa Kaunti wa Nyamira tutarudi hapa tukiwa na eneo Bunge na wawakilishi watano na sio wane. Pia nafurahi sana kwamba Kipengele 11 sasa kinaongea kuhusu maneno ya kilimo. Ni kwamba wakulima wetu wa chai sasa watashughulikiwa na Serikali. Kule Nyamira, ukishughulikia mkulima wa chai na uhakikishe kwamba anapata mapato yake vyema haswa malipo ya chai ikiwa imewekwa kwa Kshs50. Sisi ndio tutakuwa mbele katika huu wimbo wa reggae kuliko watu wengine nchini Kenya. Tunashukuru Serikali yetu kwa kuhakikisha kwamba kutakuwa na mikakati ya kushughulikia mahitaji ya wakulima wa chai, ili wasiendelee kugandamizwa. Inafaa tufuate yale ambayo Rais alituambia katika Hotuba yake; kwamba, tumalize hali ya umasikini ili Wakenya wapate mapato ambayo yanawafanya waonekane kama binadamu. Ni lazima tushughulikie mkulima. Bw. Spika wa Muda, hata ukiangalia maneno ya kilimo ya mimea kama kitunguu, wakulima hawapati soko la bidhaa yao. Hii kwa sababu wale wakulima kutoka Tanzania ndio wanaleta vitunguu kuuza katika soko letu hapa Kenya. Ukiangalia upande wa mayai, mayai mengi ambayo tuko nayo hapa Kenya yanatoka kule nchi jirani ya Uganda. Ni sharti tuweke mikakati ya kuhakikisha kwamba tunamtetea mkulima. Bw. Spika wa Muda, kule Marekani wakati hili janga la COVID-19 lilitokea, yule Rais ambaye anaondoka; Bw. Trump, aliweka kando karibu USD19 bilioni ili kuhakikisha kwamba hasara kwa mkulima inapunguzwa. Hapa Kenya pia ningeomba kwamba Serikali iweze kuweka mikakati ya kusaidia mkulima ili kupunguza hasara ambayo inawezakutokea na hili janga la Coronavirus disease (COVID-19). Bw. Spika wa Muda, katika usambazaji wa umeme, namshukuru Rais vile alituambia kuwa Wakenya wengi sana sasa wamepata nafasi ya kupata umeme. Tangu Serikali ambayo tuko nayo sasa ichukue hatamu ya uongozi, kuna maeneo kadhaa ambayo yamefaidika sana na kuunganisha umeme kwa wananchi wa nchi yetu ya Kenya. Shida ambayo iko ni kwamba ile kampuni ambayo inashughulika maneno ya kuunganisha umeme kwa wananchi, yaani, Kenya Power Company haina uwezo wa kuwafikia Wakenya wote. Hata sehemu ambazo imewai kuunganisha Wakenya saa zingine kukiwa na kasoro katika ile mitambo ambayo inasambaza umeme ambayo tunaita transformer, inachukua muda mrefu sana kurekebisha mitambo hiyo ama kuleta ingine mpya wakati inaharibika. Bwana Spika wa Muda, kwa mfano, kule eneo Bunge langu la Mugirango Kaskazini katika Kauti ya Nyamira kuna transformer ambayo iliharibika karibu miezi miwili iliyopita. Ni kule katika shule moja inaitwa Gekendo, karibu na Soko la Obwari. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}