GET /api/v0.1/hansard/entries/1037074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037074,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037074/?format=api",
"text_counter": 442,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Hii ni kwa sababu hii kampuni ya Kenya Power Company hata kama tumeipatia jukumu la kuunganisha umeme kwa Wakenya, imeonyesha wazi kwamba haina uwezo. Wakati umewadia ambapo inatakikana tukubali kwamba kampuni ingine ije ili iweze kusaidia katika hii shughuli ya kuunganisha umeme katika maeneo mbali mbali katika taifa letu la Kenya. Bwana Spika wa Muda, katika maneno ya kupigana na umasikini na upweke kwa vijana, namshukuru Rais vile amesema sasa hivi hapa Kenya tuko na wale vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda . Wanazidi sasa million moja nukta nne. Hao vijana wenyewe wanaleta katika uchumi wa taifa letu karibu Kshs357 bilioni. Lakini pia kuna shida ambayo inawakumba hawa vijana. Hawa vijana katika zile sehemu za mashambani--- Seneta wa Kaunti ya Nairobi anaweza kutueleza, lakini kule mashambani wanasumbuliwa sana na maaskari. Mara nyingi hao vijana wakiwa wanafanya biashara zao wale askari ambao wameweka vizuizi barabarani wanawaitisha Kshs50 kila wakati wanapopita katika vile vizuizi. Bw. Spika wa Muda, vile Rais amesema, angetaka kuona kwamba hao vijana uchumi wao iweze kuinuka siku zijazo wawe hata na makampuni ya kutengeneza bodaboda. Lakini itakuwaje kwamba ile juhudi ambayo Serikali yetu inaunga mkono sana inawekewa pingamizi na maaskari wetu? Nataka kuomba Serikali yetu ihakikishe kwamba wale maaskari ambao wako katika mabarabara zetu kazi yao isiwe kusumbua wale vijana ambao wanafanya kazi ya"
}