GET /api/v0.1/hansard/entries/1037076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037076/?format=api",
"text_counter": 444,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": ". Bw. Spika wa Muda, nataka nikuambie kwamba hata Ijumaa iliopita nilikuwa katika Kaunti yangu ya Nyamira nikitembea kutoka soko moja inaitwa Ikonge, nikatokea katika barabara nyingine inatokea katika kampuni ya Kipkebe. Hapo kati kati, kuna maaskari wameweka kizuizi. Hao vijana wanasema kuwa kila mara wanapopita pale wanatoa kodi ya Kshs50. Wengine wanatoa Kshs100. Huo sio ungwana kabisa. Baadhi ya vijana hao wamesoma sana lakini wanafanya kazi ya boda boda kwa sababu Serikali yetu haijaweka mikakati ya kutosha ya kupata ajira ya kutosha kwa vijana wetu. Bw. Spika wa Muda, naomba Mkuu wa idara ya polisi ahakikishe kwamba mambo ya kutesa hawa vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda ikome kabisa. Sio ungwana tena kuona vijana kama hao ambao wanajaribu kutafuta riziki kwa familia zao-- -"
}