GET /api/v0.1/hansard/entries/1037081/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037081,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037081/?format=api",
    "text_counter": 449,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nimefurahi sana na hiyo taarifa ya kujulishwa na Seneta wa Nairobi. Kwa hakika ni aibu sana kuona kwamba maaskari wetu ambao wanatakikana kutulinda na kuhakikisha kwamba wale wanafanya biashara hawatishwi, ndio wanawatesa vijana wetu. Nafikiri kama Mwenyekiti wa Kamati wa Haki wiki ijayo sisi tutafunga safari hadi ofisi ya Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC). Hii ni ili tujue ni jitihada gani zitawekwa na ile ofisi kuhakikisha kwamba maaskari wetu ambao wako katika barabara zetu na vizuizi hawawatesi vijana wetu wa boda boda . Bw. Spika wa Muda, hii ni kwa sababu hakuna haja ya kukubalia kitengo cha polisi kuwatesa vijana wanaoletea nchi yetu Kshs357 bilioni. Ni lazima tumuite Mkuu wa polisi na kitengo cha kupigana na ufisadi watueleze ni mikakati gani wameweka kuhakikisha kwamba hawa vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda hawaendelei kufanyiwa dhulma na polisi katika vizuizi. Nikiendelea pia nataka kumshukuru Rais. Amesema kwamba hii shughuli ya BBI vile tunaendelea mbele tukubali kwamba tuzungumze kama Wakenya. Mheshimiwa Rais ametuambia kwamba ile sheria ambayo imechapishwa na kuwasilishwa katika Bunge la Taifa ya kushughulikia maneno ya kura ya maoni--- Amesema kwamba tuangalie sheria hiyo ili tuweke mikakati ya kusaidia taifa hili kuenda mbele na kufanya kura ya maoni. Bw. Spika wa Muda, tangu tupitishe Katiba yetu ya 2010, nchi hii haijawai kufanya kura ya maoni. Hii ndio mara ya kwanza kabisa tunaenda katika kura ya maoni. Mheshimiwa Rais ametusihi kwamba hii sheria ya kura ya maoni ikija kwetu, tuingalie na tuifanyie ukarabati kabisa. Tuwape Wakenya nafasi watueleze ni vipi tunaweza enda kwenye kura ya maoni tukitumia sheria hii. Ningeomba Maseneta wenzangu kwamba tuangalie vile nchi zingine zinafanya. Mwaka 2008 nilipokuwa mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria nchini, nilisafiri mpaka kule Marekani wakati kulikuwa kunafanywa uchaguzi kule. Niliona kwamba katika uchaguzi wao, vile wanafanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi, pia unapata kwamba kuna maswali pale yamewekwa ya kura ya maoni. Bwana Spika wa Muda, ukitembea katika kule nchi ya Australia, wananchi wanapewa nafasi ya kufanya mjadala. Swali ya kura ya maoni ikiwekwa kwenye wananchi wanapewa nafasi ya kuchagua. Nataka niwaombe machifu wetu na manaibu wa chifu kwamba hii maneno ya kura ya maoni inaungwa mkono na Wakenya wengi. Hakuna haja hawa manaibu wa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}