GET /api/v0.1/hansard/entries/1037082/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037082,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037082/?format=api",
    "text_counter": 450,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "chifu wajaribu kuwadhulumu Wakenya wenzao. Hii sheria tutaenda kule na kuongea na watu wetu kule tunatoka na tutaipitisha kwa amani. Hatutaki Wakenya washurutishwe. Huu ni mjadala ambao uko na wafuasi wengi. Tungetaka Wakenya wapewe nafasi yao waweze kuchukua hatua ya kidemokrasia. Kuna wengi ambao wataipigia kura. Kuna wale wanaoipinga, ambao nafikiri ni wachache. Wakiikataa basi hiyo pia ni demokrasia. Tumepata eneo Bunge mpya katika jimbo la Nyamira. Tumeambiwa kuwa mambo ya wakulima wa majani chai watashughulikiwa. Kwa hivyo, tutaungana na Wakenya wengine kuhakikisha kwamba tunawapatia wetu nafasi ya kusoma vitabu vya the Building Bridges Initiative (BBI). Wakiona kwamba wanafurahishwa na wanafaidi kutokana na mapendekezo yote kama kuongeza pesa kutoka asilimia 15 hadi 35 katika Majimbo, waunge mkono. Wakiona kwamba ni vizuri kwa sababu tumeweka maneno ya Ward Fund katika Katiba, watasoma na wakiona kuwa ni sawa watapiga kura. Hiyo ni demokrasia. Kwa kumalizia, Hotuba ambayo Rais alitoa inatupa changamoto kama taifa kuunga Rais wetu mkono kuhakikisha kuwa Kenya inasonga mbele ikiweka Wakenya pamoja. Nimefurahi jinsi Rais alivyosema kuwa tumerahisisha maneno ya kusajili kampuni. Kila siku tunasajili zaidi ya kampuni 300. Shida ambayo tuko nayo ni kuwa wale wakuu wa majimbo, magavana, hawapatii vijana na kina mama wetu nafasi ya kufanya biashara. Unakuta kuwa wamama na vijana wamefanya jitihada ya kusajili kampuni zao lakini ukienda kwa serikali ya majimbo uulize vijana au wamama wangapi wamepewa nafasi ya kufanya biashara katika kaunti hakuna. Wale wachache ambao wamefanya biashara wakienda kutafuta malipo yao wanaambiwa watoe rushwa, inaitwa ‘ 10 per cent.’ Masenata, tunafaa kuweka mikakati zaidi ya kuhakikisha kuwa vijana wetu wanapewa nafasi ya kufanya kazi. Wale wawakilishi ambao wana ulemavu wameniuliza kule Nyamira kuwa hawapewi nafasi. Wanasajili kampuni zao lakini wakienda kwenye serikali ya Kaunti ili wapewe biashara, wanazungushwa huku na kule. Nafikiri ni vizuri tuitishe orodha katika kaunti zote 47 tuangalie watu ambao wako na ulemavu wamepewa nafasi ya kufanya biashara. Sheria inasema kuwa asilimia 30 ipewe vijana, kina mama na watu walio na ulemavu. Magavana wetu lazima wafuate sheria kwa sababu hayo ndio madhumuni yetu kama taifa la Kenya. Tunapoelekea Krismasi, na jinsi Rais amesema kuwa tujaribu tuwe na nchi ambayo ina umoja, tunafaa kukubali kuwa Wakenya wote wako pamoja. Tunaposhughulikia mamboa ya BBI, inafaa kutuunganisha tuendelee na tukubali kuwa nchi yetu ni moja. Rais alisema katika Hotuba yake kuwa referendum nyingi zitakuja. Hii ni moja ambayo yeye na Raila Odinga wamependekeza. Kuenda mbele, amesema kuwa kutakuwa na kura ya maoni nyingi. Nchi itazidi kubaki na ubadilishaji wa Katiba utakuja leo, kesho na siku zijazo. Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono kwa moyo wote Hotuba ya Rais wa Taifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}