GET /api/v0.1/hansard/entries/1037149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037149,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037149/?format=api",
"text_counter": 517,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ripoti ya Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Kibinadamu katika Seneti. Kwanza naipongeza Kamati hii kwa kukaa kwa muda mchache na kuja na Ripoti ambayo ina ufasaha makubwa. Itakumbukwa kwamba Kamati hii ina Wakili Waandamizi watatu ambao ni Sen. Omogeni ambaye ni Mwenyekiti, Sen. Amos Wako ambaye alikuwa Mkuu wa Sheria na Sen. Orengo ambaye pia ni Senior Counsel. Vile vile, Kamati hii ina mawakili wengine watatu wakiwamo Sen. Dullo ambaye ni Deputy Majority Leader, Sen. Mutula Kilonzo Jnr. ambaye ni wakili mwenye tajiriba kubwa na Sen. Iringu Kang’ata, Kiranja wa Walio Wengi katika Seneti. Naelezwa kuwa Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Kudumu ya Haki, Mambo ya Kisheria na Haki Za Binadamu, Sen. Cherargei, ni mwanafunzu wakili ambaye aliapishwa juzi. Nachukua fursa hii kutoa pongezi zangu kwa Sen. Cherargei baada ya kuapishwa rasmi kama wakili wa Mahakama ya Kenya. Nilipitia mafunzo hayo miaka 29 iliyopita itakapofika 19 December 2020. Kamati iliangazia vipenge kadha vya Katiba ikilinganishwa na mapendekezo ambayo yalitolewa na Kamati ya Building Bridges Initiative (BBI). Jambo la kufurahisha ni kuwa katika Mswada ambao umechapishwa rasmi wa maswala ya mabadiliko ya Katiba, mchango wa Seneti umeonekana---"
}