GET /api/v0.1/hansard/entries/1037154/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037154,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037154/?format=api",
"text_counter": 522,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "tulitoa mchango wetu kuona kuwa Seneti inabaki kuwa chombo muhimu cha kulinda ugatuzi katika Jamhuri ya Kenya. Mapendekezo kuwa Nairobi iwe metropolitan ya mekataliwa. Nairobi itabaki kuwa kaunti kama kaunti zingine. Tunapongeza kazi ambayo inafanywa na Nairobi Metropolitan Services (NMS) lakini utawala lazima urudi kwa wananchi. Utawala unarudi kwa wananchi ili wakati wananchi wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka. Napongeza Mswada wa BBI kwa sababu ya kutupa Kaunti ya Mombasa maeneo Bunge tatu ili kuboresha utendakazi wa wabunge katika eneo lile. Naunga mkono Ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Haki, Mambo ya Kisheria na Haki za Binadamu na naomba kwamba Bunge litapitisha Mswada huo."
}