GET /api/v0.1/hansard/entries/1037193/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037193,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037193/?format=api",
    "text_counter": 561,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Asante Sana, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Kama nilivyotanguliza hapo awali, ninaunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mratibu wa Walio Wengi Katika Seneti. Hii ni mara ya kwanza kuunga Hoja ambayo ameleta kwa sababu tunaenda likizo. Nina mambo mawili tu. Kwanza ni kuhusiana na kazi ya Bunge la Seneti. Tumejaribu pakubwa kulingana na vile ambavyo tumepewa katika Ibara ya 96 ya Katiba yetu ya Kenya. Tumejaribu kufanya yale yaliyokuwa mbele yetu na yale ambayo yametendeka. Huu ulikuwa wakati ambapo uhuru wa Seneti na Bunge la Taifa uliangamizwa na Serikali ya Taifa. Ninakumbuka wakati huo ndio Mratibu wa Walio wengi katika Seneti, Sen. Kang’ata, alikuwa anafanya kazi hiyo. Nimeshukuru sana kwa kusikia Ripoti ya Kamati ya Haki, Masuala ya Sheria na Haki za Kibinadamu wakizungumziwa hapa. Wakati huo ilikuwa jambo la heshima sana kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo katika Seneti. Tumejifunza mambo mengi. Kwanza, uhuru na demokrasia ya Seneti na Bunge la Taifa lazima umepewe nafasi kwa mujibu wa Katiba ya Kenya. Wenzangu wanapofurahia viti, kama vile ndugu yangu Kiranja wa Walio Wengi katika Seneti na Viongozi wa Walio Wengi katika Seneti, wajuwe ya kwamba raha ni kidogo tu. Ni lazima waambie wale wanaoogoza Serekali ya Taifa kuwa uhuru na demokrasia wa Seneti na Bunge la Taifa lazima uheshimiwe. Pili, ni kuhusiana na ile kesi tuliopeleka katika Mahakama Kuu Zaidi Nchini. Nimefurahi kuwa uhuru wa mahakama zetu ulionekana. Bunge la Seneti limepewa nafasi bora ya kujiimarisha na kuheshimika hasa wakati tunapotunga Sheria katika Seneti na Bunge la Taifa. Siwezi kujisifu lakini wakati huo nilikuwa Mwenyekti na weledi wangu ulionekana. Ninafurahi kuwa katika historia ya Bunge la Seneti itajulikana kuwa Seneta wa Kaunti ya Nandi, Sen. Cherargei, alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Binadamu. Inaonyesha kama wangekuwa wanatumia weledi, umahiri na uongozi bora katika Kamati za Seneti, ningekuwa ninaendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo. La tatu na la mwisho, nimemsikia mwenzangu akiongea katika Hoja hii kuwa BBI inashughulikia--- Ninaomba Taifa letu la Kenya tuweze kutimiza malengo na azma ya Katiba ya 2010, ili kila Mkenya apate haki. Kama tutatekeleza Katiba hiyo asilimia mia kwa mia, hatutakuwa na haja ya kuja na mchakato wa BBI ambapo watu wengine hawajakubali kuwa wameshindwa katika uchaguzi. Ninapoona Mwaka wa 2023 na kwenda mbele, tumeanza kasumba ambayo haitakuwa nzuri katika demokrasia ya taifa letu la Kenya. Wale watakaoshindwa katika uchaguzi wa urais ama uchaguzi mwingine, watakuwa wanatumia handshake ama maridhiano kama njia ya kuingia katika uongozi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}