GET /api/v0.1/hansard/entries/1037219/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037219,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037219/?format=api",
    "text_counter": 587,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "ya ugawaji wa rasilimali za kitafia kwa serikali za ughatuzi na Serikali Kuu. Hii itachangia pakubwa maendeleo katika kaunti zetu. Kaunti ya Mombasa, ambayo ilikua inpoteza takirban Kshs700 millioni sasa imebahatika na kupata Kshs1 billioni zaidi katika mgao wa 2021/2022. Bw. Spika wa Muda, pia ningependa kughusia hali ya nchi ilovyo kwa sasa. Sasa tunapambana na janga la Korona, tumeona kwamba huu mlipoko wa pili umekuja kwa kasi. Watu wengi wamepoteza maisha yao kuliko katika mlipuko wa kwanza. Huu mlipuko wa pili umeonyesha dhahiri shahiri kwamba kaunti nyingi hazikuwa zimejitayarisha. Walipaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa. Wengi hawakuwa wamejitayarisha. Vifaa vingi vilikua duni. Hakuna ventilator na vifaa vya Intensive CareUnit (ICU). Kwa hivyo, watu wengi wamepoteza maisha kwa sababu ya utepetevu wa serikali za kaunti na serikali kuu. Ipo haja ya kuhakikisha kwamba kazi yetu ya kuchunguza na kuhakikisha kwamba tunafanya uangalizi ya kisawasawa kama Bunge la Seneti unaendelea katika mwaka ujao kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kuhakikisha kwamba wananchi wanapata faida kwa kuwepo kwa Bunge la Seneti."
}