GET /api/v0.1/hansard/entries/1037220/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037220,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037220/?format=api",
"text_counter": 588,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bado kuna visa vya maafisa wa polisi kula hongo na kusumbua wananchi hususan wale wanaosafiri. Kwa mfanao, katika Barabara Kuu ya kutoka Mombasa kuenda Lamu, kuna vizuizi karibu ishirini ambazo zinachangia kuongezeka kwa gharama ya kufanya biashara katika nchi yetu. Madereva hawawezi kupita vizuizi katika barabara zetu bila ya kuwacha chochote. Utaona pia kuna ubaguzi katika kusimamisha magari katika vizuizi hivyo. Kwa mfano, magari yanayobeba miraa na bidhaa zingine za haraka zinakubaliwa kupita kwa haraka bila kuzuiliwa kama bidhaa za kisawasawa zinazoenda kuwafaidi watu wa Lamu."
}