GET /api/v0.1/hansard/entries/1037227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037227,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037227/?format=api",
    "text_counter": 595,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Temporary Speaker",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Sen. (Dr.) Mwaura): Ilidhihirika kwamba Sen. Orengo anaweza kuzungumza vyema katika Lugha ya Kiswahili. Nimeweza kuona kwamba tangu tuanze kuzungumza katika lugha ya Kiswahili katika Bunge la Seneti, watu wengi ambao walikuwa wanadhani kwamba hawawezi kuzungumza katika lugha ya Kiswahili wanazungumza katika lugha hiyo kw ufasaha. Fauka ya hayo, Bunge la Kitaifa pia limetuiga sisi kwa sababu wameweza hata kuzindua kanuni za kudumu katika lugha ya Kiswahili iliyokuwa idhana ya Bunge la Seneti lakini wakakimbia na kuzindua kanuni zao za kudumu katika ya Kiswahili kwanza. Tunaendeleza vikao vya Bunge la Seneti katika lugha ya Kiswahili hivyo Wakenya wengi wanaweza kufuata mijadala kwa urahisi. Ninajua kwamba wanaonukuu mazungumzo haya katika HANSARD wana changamoto lakini ninaimani kwamba tutaendelea kukuza ufasaha wetu wa lugha ya Kiswahili. Ingekuwa bora pia kama ratiba ya shughuli ya Bunge ingeweza kufasiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ninapata shida sana ya kufasiri kutoka lugha ya Kingereza mpaka lugha ya Kiswahili. Nimejizatiti sana kufanya ufasiri lakini ni vyema kuwa na tafsiri rasmi kwa sababu hii ni lugha ya taifa na wala sio lugha ya Sen. Mwaura. Hivi sasa ningependa kumpa Sen. Madzayo nafasi ya kuzungumza."
}