GET /api/v0.1/hansard/entries/1037229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037229/?format=api",
    "text_counter": 597,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, mimi naunga mkono kwa mara ya kwanza Mratibu wa Waliowengi ya kwamba watu waende likizo. Likizo ni kwa sababu ukifanya kazi kwa muda, binadamu yeyote lazima apate nafasi ya kupumzika, hususan wakati huu wa krismasi. Ni wakati wa kujumuika katika familia na watu wengi pia kuwa pamoja. Lakini katika ile hali ya kuwa pamoja tuweze kuzingatia haswa zaidi mambo ya Coronavirus disease (COVID-19). Tuangalie kwa sababu hili janga la COVID-19 limetokea katika Kenya ama ulimwengu mzima baada ya karibu karne nzima ya miaka 100. Bw. Spika wa Muda, hivi sasa Bunge la Seneti linaenda likizo na mimi naunga mkono. Tukiwa katika likizo yetu, ni kama vile hawa viongozi wetu wanaotuongoza katika taifa letu la Kenya, hususan Mheshimiwa Uhuru Kenyatta Rais wa Jamhuri ya Kenya na ndugu yake, Baba Raila Amollo Odinga. Waliweza kufanya “Handshake ” na hatimaye kuzindua kupeana pambaja na mkono. Halafu tukasonga mbele zaidi na kusema kwamba kunao umuhimu kuleta Wakenya pamoja. Kama tutaleta Wakenya pamoja, ni jukumu letu kuwa na kitu kama daraja. Na ile daraja wakaita BBI. Sasa ni kujenga daraja ya kuona Wakenya wote wasiangaliane kwamba huyu ni Mkikuyu, Mgiriama, Mjaluo, Mkamba, Mkisii, Maasai na kadhalika. Bw. Spika wa Muda, kwanza nampa heko sana ndugu yangu huyu Maasai, Sen. Olekina. Alitaka kufukuzwa hapa ndani. Aliye uliza swali hilo pia alikuwa ni huyu Kiranja wetu akitaka kujua kama alikuwa amevaa sawa sawa ama la. Lakini namshukuru Spika wetu Mhe. Kenneth Lusaka. Alisimama kidete na kusema amevaa kisawa sawa. Kwa hivyo, huyu kiongozi wa Wamaasai anayevaa namna hii na anaongea sana amevaa vizuri sana. Sijui kama kuna nguo nyingine ambayo amevaa, lakini vile alivyovaa. Tunajua vile Wamaasai wanavyovaa. Huwa wanavaa mavazi haya alafu ile mambo mengine hawakuzoea tokea wazaliwe."
}