GET /api/v0.1/hansard/entries/1037231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037231,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037231/?format=api",
    "text_counter": 599,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, hakuna katiba iliyo kamili. Nataka kusema kinagaubaga kwamba hata BBI ikiwepo, sisi tutakao kuwa tunaendelea na hata tukishaenda--- Kwa vizazi vijavyo, hakuna katika ulimwengu mzima katika ambayo iko kamili. Kwa hivyo kama tunatafuta katiba ambayo iko asilimia mia moja, haitopatikana. Lakini kwa wakati huu ambao sisi ndio viongozi, ni sharti tufanye juhudi zozote ambazo mimi naunga mkono zaidi yaliyo ndani ya BBI. Yana uwezo ya kusaidia Wakenya kwa hivi sasa kuwaleta pamoja. Bw. Spika wa Muda, nikisema hivyo ni kwamba katika BBI tunaona hata katika maeneo Bunge mengine, hata Kauti ya Kilifi tunayo bahati ya kwamba tumezaana kisawa sawa kama zaidi ya watu wa Kaunti ya Murang’a. Tumepata viti nine vya maeneo Bunge. Kwa hivyo, mimi Seneta wa Kilifi nikijaaliwa na Mwenyezi Mungu nitakuwa na maeneo Bunge kama 11 inshala Mwenyezi Mungu akipenda. Kwa hivyo, naunga mkono hii BBI. Sisi sote kama Wakenya ni lazima tuwe kitu kimoja na tupendane ili Kenya iwe inaweza kuendelea mbele kimaendeleo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}