GET /api/v0.1/hansard/entries/1037233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037233,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037233/?format=api",
    "text_counter": 601,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, pia nataka kuunga mkono Bunge la Seneti kwa kusimama kidete na ile “ Team Kenya ” ambayo ilifanya vilivyo usiku na mchana, kuwe na mvua ama jua. Hatawezekana ikiwa kama Wakenya watagawanyana. Tulisema kuwa haitawezekana. Kila kaunti ipate pesa yake na hatimaye tuliweza kupata. Kwa hivyo, yale mengine ambayo tunasema yataangaliwa pole pole halafu uhusiano mwema utaendelea na kila mtu atafaidika na pesa tutakazokuwa tunapigania ziwe zinaweza kwenda katika serikali zetu za mshinani. Bw. Spika wa Muda, la mwisho ni kwamba sisi katika hizi shamra shamra, tunasema kwamba Bunge la Seneti ni lazima pia liheshimiwe. Tunaona hivi sasa bado kuna marekebisho tunahitaji. Lakini, hata kama yako, tukipitisha, tutayarekebisha alafu tuendelee kama Wakenya wa nchi moja ambao wanapendana hili nchi yetu ipate mafanikio."
}