GET /api/v0.1/hansard/entries/1037250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037250,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037250/?format=api",
"text_counter": 618,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Waheshimiwa Maseneta, mtakumbuka kwamba Kamati ya Muda ya COVID-19 iliundwa na ilikuwa ya kipekee katika Bunge zetu mbili. Kamati hiyo ilifanya kazi nzuri sana kuhakikisha kwamba imetoa mikakati na kupiga msasa miradi yote kuhusu janga hili ambalo liliendeshwa na Serikali ya kitaifa na zile kaunti. Kwa hivyo, ilitubidi kubadilisha Kanuni za Kudumu za Seneti ili tuwe na kikao cha jumla cha Kamati zetu kwa njia ya mtandao. Tunashukuru kwa sababu Kamati zetu sasa hivi zinaweza kuwa na vikao vyake kupitia mtandao, lakini ukiangalia Sehemu ya 29(a) ya Kanuni za Kudumuza Seneti hatukuweza kuwafikia lengo la kuwa na kikao cha pamoja cha Bunge la Seneti kupitia mtandao. Nataka kuwahakikishia kwamba jambo hili linashughulikiwa na Ofisi yangu."
}