GET /api/v0.1/hansard/entries/1037251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037251/?format=api",
"text_counter": 619,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Waheshimiwa Maseneta, jambo ambalo lilikuwa la muhimu sana katika awamu hii ya nne ni kwamba tuliweza kupitisha Mgao Wa Tatu wa Fedha katika serikali gatuzi na Ratiba ya Ugavi wa fedha kupitia Mswada huu kwa serikali zote 47 za gatuzi. Sote tunakumbuka kuafikiana kwa mgao huo halikuwa jambo rahisi. Tulikuwa na tumbojoto kila wakati tulijaribu kugawa pesa kwa kaunti zetu. Maseneta walizomeana. Wakati mwengine tulikuwa na dosari kama jambo hili lingewezekana. Tulikuwa na vikao zaidi ya kumi. Lakini kwa uvulivu wetu, kuwa na subira na kuelewena, Waheshimiwa Maseneta walifikia azimio la pamoja na kupitisha fomula ya huo Mgao wa Tatu na Ratiba Rasmi ya Ugavi wa Fedha kwenye serikali gatuzi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}