GET /api/v0.1/hansard/entries/1037254/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037254,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037254/?format=api",
"text_counter": 622,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Uamuzi huo wa kihistoria wa Mahakama Kuu umeweza kuzindua na kuumbua upaya namna ya utunzi wa sheria na kanuni za Bunge kwa ujumla. Uamuzi huo umeweza kuonyesha kwamba lazima Katiba na sheria zote za Kenya zifuatwe na umeipa Bunge la Seneti hadhi ya juu hususani tukizingatia mambo yote ya ugatuzi kwa ujumla. Ni muhimu tunaposonga mbele kuhakikisha kwamba tunafuata kanuni zote na sheria zote hususan ibara hii ya 110(3) ambayo inasema kwamba lazima Maspika wote wawili waweze kuwa na hati ya kuidhinisha kila mswada kabla ya kuwasilishwa katika Bunge yoyote hususan. Hilo ni jambo ambalo linasaidia sana Bunge la Seneti kuwa na nguvu zaidi. Waheshimiwa Maseneta, nafikiri tumepiga hatua kubwa sana kuhakikisha kuwa Bunge la Seneti limeweza kuheshimiwa na naomba muwe na subira na kuelewa wakati Ofisi yangu inapofanya kazi pamoja na Bunge la Seneti na Spika wa Seneti kuhakikisha kwamba miswada hii imeweza kuchapishwa upya kulingana na ibara ya 110(3) ya Katiba yetu. Waheshimiwa Maseneta, ningependa kusema kwamba tumefanya kazi vyema kabisa katika awamu hii ya nne. Lakini nataka kusema kwamba tunapoingia katika awamu ya tano, tunahitaji sana kufikiria vile ambavyo tutakavyofanya kazi wakati hili janga la COVID-19 litakuwa limemalizika. Ni muhimu sana tufikirie vile ambavyo tunaweza kukuza uchumi wetu katika anga ya kitaifa na pia katika kaunti zetu zote na vile ambavyo tutaweza kufanya biashara yetu na kuendesha vikao vyetu vya Bunge hii na Kenya kwa jumla. Kwa sababu hii, Ofisi yangu inatumai kuwa na kikao maalum tukiwa pamoja na uongozi wa Seneti ili Maseneta waweze kufikiria vile ambavyo tutaweza kuendelea na vikao vyetu na kuendesha nchi yetu hii ya Kenya. Nataka kusema ya kwamba tutakuwa tukiwasiliana kuhusu kikao hiki kabla ya kuanza awamu ya tano. Waheshimiwa Maseneta, nachukua fursa hii kuwapatia kongole zangu kwa sababu ya kujitolea kwenyu na vile ambavyo mumeweza kuhakikisha kwamba hamjatelekeza majukumu yenyu hata kama kumekuwa na hili janga la COVID-19, na vile ambavyo mumehakikisha ya kwamba mumeweza kutimiza majukumu yenyu ya kikatiba. Tunapo amka sasa kuahirisha kikao hiki, nawatakia muwe na wakati mwema na familia zenyu, muwe na likizo njema na pia muwe na mwaka mpya wenye mafanikio wa 2021. Nawashukuru."
}