GET /api/v0.1/hansard/entries/1037938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037938,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037938/?format=api",
    "text_counter": 340,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kanduyi, FORD-K",
    "speaker_title": "Hon. Wafula Wamunyinyi",
    "speaker": {
        "id": 291,
        "legal_name": "Athanas Misiko Wafula Wamunyinyi",
        "slug": "athanas-wamunyinyi"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii. Naunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Kimunya, Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi hapa Bungeni. Naunga mkono Hoja ya kuhifadhi Miswada. Zaidi ya miaka miwili iliyopita, nilipendekeza Mswada unaohusu sukari, kwa kimombo unaitwa “Sugar Bill” ambao uliamrisha uende kwa Kamati inayoshughulika na mambo ya kilimo ili iweze kufanya public participation, yaani kusikiliza na kuchukua maoni ya wananchi. Mswada huu umekaa kwa Kamati hiyo zaidi ya mwaka moja na nusu. Nilitoa lalama kwako kuwa kamati za Bunge hazifai kuweka Miswada Binafsi iliyoletwa na Waheshimiwa kwa muda mrefu sana mpaka ilazimike ziokolewe na HouseBusiness Committee . Naomba Wenyekiti wenzangu na Wabunge katika kamati za Bunge wawe wakitekeleza wajibu wao muhimu wa kuhakikisha wanajadili na kupitisha Miswada, na kuwasilisha ripoti zao Bungeni ili zifanyiwe legislation inayofaa. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii. Naamini tukirudi baada ya likizo au wakati wowote tutakapoitwa kwa special sitting, tutaomba tukubaliwe kuleta hii Miswada iliyokaa siku nyingi. Ahsante."
}