GET /api/v0.1/hansard/entries/1042949/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1042949,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1042949/?format=api",
"text_counter": 729,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, ningependa kutuma rambirambi zangu na za familia yangu na watu wote wa Laikipia kwa familia ya mwendazake Sen. (Dr.) Kabaka, pamoja na watu wa Machakos. Jambo ambalo ninakumbuka kuhusu Sen. (Dr.) Kabaka ni kwamba alikuwa mtu mkarimu sana. Ninakumbuka wakati ndugu yetu, mwendazake Sen. Oluoch, alipotuacha, Sen. (Dr.) Kabaka alijitolea kulipa karo ya wanafunzi wa mwendazake. Ninakumbuka aliandika hundi ya kusaidia. Ukarimu wake ulijitokeza vizuri sana. Ninamkumbuka kama msomi. Tulisafiri naye katika nchi ya Australia. Tulipokua huko, aliniambia kitu kizuri zaidi. Alienda kwenye maktaba na akanunua vitabu vya wanasheria. Ni mtu aliyejulikana sana kwa mambo ya masomo. Jambo lingine ambalo nina jua ni kwamba alikuwa mtu stadi sana katika mijadala ya Seneti. Kwa hivyo, tutamkosa sana. Jambo lingine lililojitokeza kwa Sen. (Dr.) Kabaka ni kwamba alikuwa na msimamo dhabiti. Mimi nilikuwa nikimrai ateme ‘ Team Kenya’ na ajiunge na timu yetu ya “ one man, one vote, one shilling,” kwa sababu kaunti yake ilikuwa imeongezewa pesa. Lakini alisimama kidete na kusema kuwa hawezi kuwaacha ndugu zake kutoka Makueni na Kitui. Ni mtu ambaye akisema jambo, analisimamia kwa ustadi sana. Yeye ni rafiki yangu na rafiki wa wengi hapa. Tutamkosa sana. Safiri salama."
}