GET /api/v0.1/hansard/entries/1043197/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1043197,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1043197/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa kuzuia madawa ya kutitimua misuli katika michezo. Kwanza, kabisa, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia ya mchezaji wetu mmoja kwa jina maarufu Ali Kajo, ambaye alifariki jana Mombasa. Marehemu Ali Kajo ni mojawapo aliyecheza na marehemu Joe Kandenge, James Yanga, Farah Ahmed na wengineo ambao waliletea nchi hii sifa nyingi katika miaka ya 1960. Marehemu Ali Kajo na wenzake walishinda Gossage Cup mwaka wa 1965 na kuiweka nchi yetu ya Kenya katika zile nchi ambazo zilikuwa zimebobea kwa kandanda. Nachukua fursa hii kutuma rambi rambi zangu kwa familia, ndugu, marafiki na wachezaji mpira wote wale wa zamani na wa sasa. Wakati wa zamani, ilikuwa nguvu zako binafsi ndio zilikuwa zinatumika zaidi katika michezo yote. Wachezaji walikuwa wanaaminika kwa sababu wengi hawakupatikana na shida ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu au kusisimua misuli. Bw. Spika, naunga Mswada huu mkono kwa sababu umekuja wakati mwafaka tukiona kwamba katika ulimwengu, tunaingia katika awamu nyingine ya kupambana na madawa za kusisimua misuli. Nchi za ulimwengu zitakuwa na sheria mpya katika mwaka wa 2021 na sisi Wakenya hatutaachwa nyuma kwa sababu tukiachwa nyuma ina maana kwamba wanamichezo wetu wengi watafungiwa nje. Hatutaweza kuruhusiwa kushiriki katika michezo ya ulimwengu ambayo inaletea nchi yetu sifa na pesa za kigeni ambazo ni haba sana katika nchi yetu ya Kenya."
}