GET /api/v0.1/hansard/entries/1043209/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1043209,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1043209/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kuna wadau wengi ambao walilalamika kwamba hawakuhusiswa katika kura zile. Walikimbilia Sports Tribunal, lakini ilikiuka amri ambayo walikuwa wametoa awali kuhusiana na swala lile lile. Walisema kwamba kura inaweza kuendelea licha ya kwamba Sports Registrar alikuwa amesema kwamba FKF haijatekeleza yale masharti ambayo yalikuwa yamewekwa kama sheria kuhakikisha kwamba wanafanya uchaguzi ambao ni huru na wa haki. Bw. Spika, mbali na kuangazia wachezaji ama wanamichezo ambao wanahusika katika michezo moja kwa moja, iwapo tunataka kukuza michezo na kuinua vipaji katika nchi yetu, kuna haja ya kuangazia hizi federations kama vile utendakazi wao na jinsi wanatumia fedha. Bw. Spika, kulikuwa na tuhuma hapo awali kwamba pesa zinazokuja za FIFA za kukuza michezo, yaani, youth development, ili kuangalia michezo ya under 17, under 19 na under 1--- Hata hivyo ifikapo mwisho wa mwaka, hakuna hata kitu kimoja ambacho kimefanyika kuhakikisha kwamba michezo ile inainuka. Bw. Spika, kuna haja muhimu kabisa. Hii ni kwa sababu michezo inawapa matumaini watu wengi. Kwa mfano, vijana wengi hivi sasa wanaingilia mihadarati kwa sababu hawana nafasi ya kucheza michezo. Tukiangalia viwanja vyetu vya michezo, michezo kama basketball imeweza kufa katika miji mingi kwa sababu hatuna viwanja vya kutosha kuhakikisha watu wanafanya mazoezi na wanaendelea na michezo yao. Bw. Spika, kuna haja tuangalizie hizi federations pia. Hii ni kwa sababu hii sheria inamlenga yule mwanamichezo binafsi kuhakikisha kuwa akikimbia ama kufanya mchezo wake, asiwe ametumia madawa ya kulevya ama madawa ambayo yanatumika kusisimua misuli. Tuangalie pia hizi federations zinatumia vipi fedha zinazotoka, yaani"
}