GET /api/v0.1/hansard/entries/1044191/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1044191,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1044191/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Richard Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ", (Kitutu Chache South, FORD-K): Thank you Hon. Speaker. Ningependa nizungumze kwa Kiswahili. Pole kwa kuanza kuzungumza kwa Kiingereza. Ningependa kusema kuwa Mzee Nyachae ni mzee ambaye anaheshimika kwa jamii ya Mkisii. Mzee Nyachae alifanya kazi na hayati Mzee Moi na bahati yangu ni kuwa Mzee Nyachae alifanya kazi pia na baba yangu ambaye alikuwa Mbunge hapa; Mzee Dkt. Zachary Onyonka. Wakati mke wa Mzee Nyachae alifariki mwaka uliopita, niliona ni heshima kubwa kwenda pale nimzungumzie huyu mzee. Hii ni kwa sababu nilikuwa sijamzungumzia tangu miaka kumi na mitano iliyopita. Nilipoenda kumzungumzia kabla ya mazishi, aliniambia kuwa: “Unajua mimi na baba yako tulikuwa na mvutano wa vuta nikuvute, lakini ule ulikuwa ni mvutano wa kiume lakini wa kiheshima. Hatukuwa na matusi. Tulikuwa na njia na fikira tofauti vile Kenya inafaa kuendelea ama hata jamii ya Mkisii. Lakini heshima nilimpa baba yako naye alinipa heshima ijapokuwa tulikuwa wapinzani.” Mhe. Spika, juzi nilikuwa na furaha yule mzee kuniambia kuwa kwa maisha yake ya mwisho hakuwa na shida na familia ya Mhe. Dkt. Onyonka. Kwa hivyo, ningependa kusema hapa katika hili jumba ya kwamba Mzee Nyachae aliheshimika Kenya nzima. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}