GET /api/v0.1/hansard/entries/1044192/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1044192,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1044192/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Richard Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ninyi viongozi mlioko hapa haswa wakati huu ambapo nchi yetu inahitaji watu ambao wana roho safi, akili timamu na wana nia njema kwa nchi yetu, tujaribu kujadiliana na kuzungumza kati yetu ili tusije tukasukuma nchi yetu ikaenda mrama. Ningependa kusema kuwa Mungu amuweke mahali pema peponi huyu Mzee. Tutaiombea familia yake. Tunatarajia kuwa hata kama watakuwa na mambo fulani mazito mazito, mzee alikuwa na marafiki chungu nzima. Kwa hivyo, familia yake waendelee kuzungumza wakubaliane kwa sababu jina la Mzee Nyachae lataka liachwe kule juu ambako mashujaa wa nchi ya Kenya…"
}