GET /api/v0.1/hansard/entries/1044401/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1044401,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1044401/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "hawa Maseneta wote ni watu ambao wamefaulu katika nyadhifa zao kwa muda wa miaka mine. Wameweza kudhibitisha umahiri wao katika kazi zao. Jambo la muhimu ni kwetu sisi sote kuzingatie mambo ya wananchi. Wananchi wa Kenya wako na imani sana na Bunge la Seneti kwa sababu ya hoja na miswada ambayo imeweza kuletwa mbele ya Seneti na kujadiliwa kwa kina. Maseneta ni viongozi ambao wanajiheshimu. Sisi si watu ambao tunaweza kupigana mandondi mbele ya wananchi. Tumejiwekea heshima na ninatumaini tutaendelea hivyo. Nataka niwapatie pia kongole Maseneta kwa kuweza kuweka kielelezo cha kwamba kama mnataka Bunge liheshimiwe, basi nyinyi muwe kama sisi Maseneta hapa. Bw. Spika, nataka tutambue uwepo wa Maseneta ambao tunawaita Maseneta wakongwe ambao wameweka heshima yao katika utendakazi. Tukiangalia sisi katika haya Mabunge mawili tunapata ya kwamba katika Bunge la Seneti ndio kuna Maseneta ambao wamebobea. Tuko na Sen. Wako ambaye hata hana haja ya kuongea kwa sababu anaweza kuchambua sheria vile inavyotakikana. Tuna pia Sen. Omogeni na ndugu yetu Sen. Orengo na Sen. Murkomen ambao ni weledi wa sheria. Pande hii tukiwa na Sen. Mutula Kilonzo Jnr., akiiga mfano wa babake Marehemu Mzee Mutula Kilonzo Snr. Kwa hivyo, Bunge la Seneti liko watu kadhaa ambao wako na uwezo wa kufanya shughuli hii bila kujali malipo. Bw. Spika, utaona ya kwamba, katika utendakazi wa mawakili ulimwengu mzima, wanavaa gauni nyeusi na si ile ya aliyekuwa Jaji Mkuu Mutunga ile ya kijani. Wanavaa gauni ile nyeusi na utaona kuna kitu kinatembea kwa mgongo. Hicho ni kama kipochi. Zamani mawakili walikuwa hawawezi kuitisha pesa lakini wakifanya kazi ya kusaidia jamii. Hapa hawa mawakili wetu walijitolea kusaidia Bunge la Seneti ili kuweka kilelezo cha wale watakaokuja nyuma yetu kama Maseneta; kongole sana ndugu yangu Sen. Omogeni, Sen. Mutula Kilonzo Jnr., Sen. Orengo na wengineo walioweza kushirikiana na baadhi ya hawa mawakili kuweza kupigana huko ndani ya koti. Hatimaye tuliweza kushinda zile sheria ambazo zilipitishwa bila ruhusa ama majadiliano hususan wewe na wale wanaohusikana na hizo sharia ambazo zilipelekwa kwa Rais na zikatiwa kidole kinyume cha sheria. Hawa walifanya juhudi na hivi sasa inabainika wazi ya kwamba hakuna chochote kitapitishwa ndani ya Bunge la Kitaifa ambacho kinahusikana na mambo ya ugatuzi bila kupitia hapa. Hiyo ni heko kubwa sana. Siko hapa kusema kwamba pengine walipwe. Hapana. Lakini kuna ile tunaita imani pia ni kutiana moyo. Jambo kama hili ni kama ile ambayo tunafikiria ama tutaona ama wewe mwenyewe ukiketi katika ile hali yako ukiona ikiwa wanafaa. Wao hawatakuuliza. Kile kifugo kiko hapa nyuma ya zile koti, wewe enda ukaweke vile unavyofikiria halafu wataenda zao na watakupatia shukrani. Bw. Spika, la mwisho ni kuhusu hoja na miswada ambayo tunaleta katika Bunge hili. Ni lazima tuhakikishe kwamba wananchi tumewapatia kipaumbele katika hoja na miswada yetu ile tusifanye vitu ambavyo vitaweza kuleta mtafaruku. Kama sasa kuna watu ambao ukiwauliza ni kwa nini wewe unapinga BBI na hujaisoma. Hajui kumeandikwa nini, lakini atakuambia tayari mimi siitaki. Kisha katika hali ya ile The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}