GET /api/v0.1/hansard/entries/1044402/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1044402,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1044402/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "mtafaruku, pengine watu wanaweza kuanza kupigana na maisha kupotea na pengine kujeruhiwa. Kwa hivyo, tunasema ya kwamba tuwe wa kwanza kama kielelezo. BBI si jambo mpya kwetu sisi kwa sababu tuliweza kufanyia Katiba yetu marekebisho na tukapata Katiba mpya mwaka wa 2010. Sasa ni mwaka wa 2021 ambapo tunaongea juu ya BBI. Baada ya miaka 11, mambo mengi sana yamegeuka na yanahitaji kugeuzwa na kuona ya kwamba nchi hii kutakuwa na amani, upendo na watu wakiishi kwa furaha baada ya kupiga kura. Bw. Spika, kusitokee jambo mbaya ambalo litafanya mimi nianze kuchukia huyu kwa sababu ni wa kabila la Kalenjin, Mkikuyu, Mkamba au Mgiriama. Isiwe namna hiyo. Sote tuwe kama Wakenya. Tunasema ya kwamba wale wasiofahamu, lazima wapate nafasi ya kuuliza ili wapate kuelezwa. Mambo yaliyotokea mahali kama Githurai ama Burma ama kwingineko katika Taifa la Kenya, ni aibu kubwa katika mazishi watu wanazusha na wanaanza kutandikana makonde. Hiyo haifai. Aibu ndogo ndogo kama hizi, sisi tukiwa waheshimiwa, ni lazima tujiheshimu kwanza. Bw. Spika, nataka kumalizia nikisema kwamba katika wale watu walichaguliwa katika harakati zote za Bunge ambazo tutazifanya, hao ni Maseneta ambao ni wakakamavu. Ningependa kujiunga na kusema ya kwamba ni sawa kabisa. Asante."
}