GET /api/v0.1/hansard/entries/1044866/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1044866,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1044866/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika. Kuna msemo uliosemwa na Wahenga zamani kwamba ukiona cha mwezako kimenyolewa, chako anza kutia maji. Jambo hili la kuvunjiwa nyumba na Wakenya kuitwa maskwota, yaani mahali ulipokaa kwa muda mrefu kuwa si kwako, ni jambo ambalo limetendeka sana hata upande wa Pwani. Ni kitu cha kusikitisha kwamba katika makabila yote 45 sasa, Wanubi ni watu ambao tunajua kwamba wanaishi katika sehemu za Kibera na Kibos. Ijapokuwa sio wengi, inajulikana kwamba ni Wakenya wanaoishi na heshima zao kama vile jamii zingine za Kenya zinavyoishi. Kitendo cha unyama kilichotendewa Wakenya wenzetu kilikuwa cha kuhuzunisha sana. Kilionyeshwa katika vyombo vyote vya habari. Kile kitendo cha unyama kilifanywa mpaka kwa mama aliyekuwa ndani ya nyuma. Ni binadamu gani anaweza kuchukuwa trekta huku akisikia kelele ndani na mama anajaribu kumtoa mtoto wake--- Ilibidi mama atoke nje na yule dereva aliendelea kubomoa mpaka akamuuwa mtoto ambaye angekuwa wa manufaa sana katika jamii ya Wakenya katika maisha ya usoni. Ni muhimu sana sheria ichukuwe mkondo wake. Aliyetumwa hakutumwa kwenda kuuwa. Kama alitumwa kubomoa vyumba vilivyokuwa pale, angefanya hivyo kwa hali ya ubinadamu. Ubomoaji wa nyumba hizo ulifanywa kwa hali ya unyama. Unyama huu unakwenda mpaka unavunja miskiti, watu wanapokwenda kumuomba Mungu. Afadhali usivunje msikiti ama kanisa ambapo watu wanakoenda kumuomba Mungu. Wewe ni binadamu unayeishi katika ulimwengu kwa mapenzi ya Mungu. Watu wako na imani na misikiti, makanisha hata kama ni Kalasinga wanaoabudu katika hekalu zao. Ni mara yangu ya kwanza kuona msikiti wa Kiisilamu unabomolewa na tinga tinga ikisemekana kwamba ulijengwa bila haki. Tunajuwa kwamba kisheria watu wakikaa mahali kwa miaka zaidi ya 12 bila kusumbuliwa au kuambiwa waondoke, hata kama ni mahali gani, ni lazima wapewe nafasi ya kwanza kumiliki ardhi hiyo. Kibos ni eneo kubwa lenye makanisa, miskiti na nyumba za watu. Wamesema ya kwamba wamekuwa hapo zaidi ya miaka 90. Ni jambo la kusikitisha kuona hivi leo Serikali yetu, haswa Shirika la Reli ambalo liko katika hali taabani na karibu kuanguka, linaweza kuvunjia watu misikiti na nyumba. Wakati huu wa Covid-19, shirika hilo linatoa watu nje na kuwafanya walalahoi katika nchi yao ya Kenya ambapo wamezoea kuishi. Bi. Naibu Spika ninamshukuru sana ndugu yangu, Sen. Outa, kwa kuulizia Taarifa hii. Ningependa Kamati itakayoishughulikia ichukue hatua mwafaka ili kwenda"
}