GET /api/v0.1/hansard/entries/1046238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1046238,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1046238/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, nataka kumpongeza Sen. Wambua wa Kitui kwa kuleta Mswada huu. Kwa kweli, Serikali inasema tunahitaji usalama wa chakula. Kitu ambacho kitasaidia zaidi ni mimea ambayo inahitaji mvua kidogo ama maji yasiyo mengi, ili iweze kuwa katika kipaombele ya hili jambo ambalo linasemwa na Serikali. Ndengu inaweza kukuzwa katika sehemu nyingi. Sehemu nyingi za Kenya ni za ukame. Ukienda Laikipia, Isiolo, Marsabit, Tharaka-Nithi, Kitui na Machakos, ndengu inaweza kupandwa na itafanya mambo mawili. Jambo la kwanza ni kuwa watu ambao wanasema kuna ukosefu wa kazi watapata kazi ya kufanya. Jambo la pili ni kuwa ukitembea sehemu kama Laikipia ambako kuna ukame, kuna wale ambao wanafuga mifugo na kazi yao ni kuhama hama. Hao watapata kazi ya kufanya na usalama utaimairishwa. Hali ya usalama imezorota sana kwa sababu kuna watu wengi ambao kazi yao ni kupiga wengine wakitafuta mifugo yao. Lakini wakipata kazi ya kufanya, visa vya hivi vitapungua. Ndengu ni mmea ambao utahitaji siku chache sana, pengine miezi miwili na nusu ndio uweze kuvuna. Ndengu inaweza kukaa kwa muda mrefu sana bila kutumia jokofu . Ndengu inawekwa hadi ikauke na utaweza kutumia baada ya miezi mingi ikiwa pale. Jambo ambalo ningependa kusisitiza ni kuwa kaunti zetu ambazo zimepewa jukumu la kuangalia mambo ya ukulima yapewe kipaombele ili mimea, haswa ndengu, ambayo inakuwa kwa muda mchache watilie mkazo. Wakitilia mkazo, nina uhakika kwamba jambo hili litasaidia katika mambo ya usalama wa chakula. Inaweza kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}