GET /api/v0.1/hansard/entries/1046239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1046239,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1046239/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "kupigana na mchakato wa hustlers ama wanyonge au walala hoi kwa sababu watafaidika sana na sisi kama Seneti tunafaa kupitisha Mswada huu bila kupoteza wakati. Itasaidia Wakenya wengi. Nchi yetu ya Kenya itapata mapato kwa sababu watu wengi wataanza kufanya kilimo biashara. Kilimo biashara itawezekana kwa mimea ambayo haihitaji mvua nyingi, kwa sababu sehemu nyingi za Kenya hazina mvua ya kutosha. Kwa hivyo, mimi naunga mkono Mswada huu. Nataka kuambia Sen. Wambua kuwa hii juhudi ni nzuri sana. Amechelewa na angefanya hivi mwaka wa kwanza tulipoingia hapa. Hata hivyo, ni vizuri kwa sababu tunaweza kuchukua fursa hii kuleta mabadiliko katika nchi yetu ya Kenya. Itawezekana ikiwa sheria kama hizi tutazipitisha kwa haraka ndio tuweze kuwasaidia Wakenya wenzetu. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}