GET /api/v0.1/hansard/entries/1047431/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1047431,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1047431/?format=api",
"text_counter": 414,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": " Asante Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii fursa hata mimi nichangie. Nataka kuanza kwa kupongeza Kamati husika kwa kuleta huu muongozo. Natangulia kwa kusema huu ni muongozo ambao tuliuhitaji kama jana kwa sababu eneo kubwa la kaunti ambayo mimi nawakilisha, Kaunti ya Taita/Taveta, limechukuliwa na mbuga ya Tsavo. Asilimia 62 ya kaunti yetu ni mbuga ya Tsavo. Kwa hivyo, sisi kama wakaazi wa Taita/Taveta tunaiona mbuga hiyo kuwa laana na sio baraka. Sababu ambayo tunaona mbuga hiyo kuwa laana na sio baraka ni kwa sababu wanyama kutoka Mbuga ya Tsavo wametuathiri sana. Watu wengi wameuawa na wanyama. Mashamba na mimea pia imeharibiwa. Tumekuwa tukilalamika miaka nenda, miaka rudi, lakini hatujawahi pata suluhu au watu wetu kulipwa kutokana na matukio hayo. Hivi majuzi, mvua ilinyesha na watu wengi walilima lakini cha kushangaza ni kuwa hakuna mavuno kwa sababu ndovu walivamia na kuharibu. Mwongozo huu unanipa matumaini kuwa tunaweza kupata mwelekeo na mwafaka mzuri kusaidiana. Hivi majuzi kulikuwa na zoezi la kuajiri vijana kazi kwa mbuga za wanyama. Kama Kaunti ya Taita Taveta, tulitarajia kuona vijana wetu wengi wakiajiriwa kwa sababu tunaathirika sana na hii mbuga, lakini cha kushangaza ni kuwa vijana wachache tu ndio waliochukuliwa. Jambo hilo halikutufurahisha kamwe. Mambo mengi yanaweza kufanyika kuleta uhusiano mwema ili kama kaunti tuache tu kuona mbuga kama ya kutudhuru. Shirika la KWS linaweza kuwasaidia wakaazi wa kaunti ambazo ziko karibu na mbuga za wanyama kwa kujenga shule na kuwapa maji ili kuweka uhusiano bora. Nimeupitia mwongozo huu na ninafurahi kuwa utatusaidia kwa kiwango fulani. Ijapokuwa sio kamili, ni bora. Ninaunga mkono uanze kutumika ili watu wapate afueni."
}