GET /api/v0.1/hansard/entries/1047696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1047696,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1047696/?format=api",
"text_counter": 257,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mzee Haji alikuwa mtu wa msimamo kabisa hususan katika ugavi wa fedha zinazoiendea serikali zetu za ugatuzi. Wakati tulikuwa na mjadala kuhusu ugavi wa fedha mwaka jana, Mzee Haji aliniita kando na akaniambia, ‘Hivi ni vita na ikiwa kuna tashwishi zozote, wewe usiwache sababu iliyokuleta hapa; kutetea watu wa Kaunti ya Kilifi. Kufa nao na kuwa na msimamo nao wala usibanduke hata kidogo’ Maneno aliyonena Mzee Haji yalinipa nguvu sana. Ijapokuwa tulionekana kama watu wanaokosa kueleweka, ilikuwa ni kwa sababu ya msimamo tuliochukuwa. Ikiwa Mzee Haji anaweza kuchukua msimamo kama ule, itakuwaje sisi wengine kama vifaranga tusiweze kuchukua msimamo? Bi. Naibu Spika, namshukuru marehemu Yusuf Haji kwa sababu alikuwa na msimamo. Kwa ndugu zangu wa Ijara, Garissa pamoja na watu wote ambao ninawakilisha katika Seneti, husasan watu wa Kilifi, nasema poleni. Tunamwombea marehemu Mzee Haji ijapokuwa roho zetu ni nzito sana kwa wakati huu. Sisi tulimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Letu ni kumwombea tu pamoja na familia yake. Sote tunajua kwamba hiyo ni njia ya kila mtu. Tunaombea familia yake iwe na nguvu na kustahimili kumpoteza mzee. Naomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Mzee Haji mahali pema penye wema peponi."
}