GET /api/v0.1/hansard/entries/1047737/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1047737,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1047737/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Temporary Speaker",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Sen. (Dr.) Mwaura): Asante Sana, Sen. Farhiya. Ingawa umeniita “Madam Speaker” mara nyingi sana hata baada ya kukukosoa, lakini nafikiri ni kwa sababu ya jazba za kumpoteza mzee wetu, Sen. Haji. Alikuwa ni mzee wa heshima na taadhima nyingi mno ambaye hakuwa anaonyesha hisia. Alikuwa ni mwaminifu sana kwa ule upande ambao yeye mwenyewe alikuwa anaunga mkono. Alifika mpaka akaonekana kwamba yeye ndiye sura ya Serikali katika Jamhuri hii yetu ya Kenya kwa nyadhifa zote aliwahi kutumika aidha kama mkuu wa mkoa ama waziri. Kwa hivyo, ni jambo la kusifiwa sana. Kwa sababu ya hiyo, nampa nafasi sasa Kiranja wa walio Wachache, Sen. Mutula Kilonzo Jnr."
}