GET /api/v0.1/hansard/entries/1047763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1047763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1047763/?format=api",
    "text_counter": 324,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuunga maseneta wenzangu katika kutoa risala za rambi zangu na za watu wa Kaunti ya Kwale kwa kumpoteza Mzee wetu, Sen. Yusuf Haji, aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Garissa. Nilipojiunga na Bunge hili la Seneti katika mwaka wa 2017, Mzee Haji aliniita kando siku moja na kuniambia: ‘Kijana, nilifanya kazi na babako, marehemu Mzee Juma Boy, alipokuwa mbunge wa Kwale ya Kati katika Serikali ya Mzee Jomo Kenyatta na vile vile pia marehemu kakako mkubwa katika Bunge la 11 hapa Seneti.’ Alizidi kuniambia, ‘Wewe kijana una bahati sana kwamba tuko na wewe katika Bunge hili la 12 katika mwaka wa 2017. Nashukuru sana na natumahi utafuata mwendo waliochukua babako na ndugu yako’ Kwa hivyo mimi nakumbuka sana maneno aliyoniambia Mzee Haji na yale alinena katika Bunge hili la Seneti. Bw. Spika wa Muda, tulipokuwa na mjadala wa ugavi wa fedha mwaka jana, Mzee Haji alikuwa na msimamo mkali sana. Alisisitiza kwamba hakuna kaunti itakayopoteza hata ndururu katika mgao wa fedha kutoka Serikali kuu. Kwa kweli, Mzee Haji alisimama imara na tukafaulu sote katika Bunge hili la Seneti. Naomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi kwenye watu wema. Mwisho, ni lazima Serikali hii ikumbuke kumfanyia maheremu Sen. Haji kitu katika kumbukumbu yake. Kama alivyosema Sen. Mutula Kilonzo Jnr., lazima kufanywe kitu cha maana kando na kuita bara au nyumba kutajwa yeye ili ionekane kote nchini kwamba marehemu Sen. Haji alikuwa shujaa katika nchi yetu ya Kenya. Marehemu Sen. Haji alihudumu kama mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, na kisha kuwa mbunge. Marehemu Sen. Haji alifanya mambo mengi na sisi kama Wakenya ni lazima tuwe na kumbukumbu ya kumkumbuka. Nawaombea watu wa Garissa pia wawe na subira na kuwahimiza watenge sehemu au hata wajenge shule katika eneo la Garissa litakalokuwa kumbukumbu ya marehemu Sen. Yusuf Haji. Asante sana, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii."
}