GET /api/v0.1/hansard/entries/1047790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1047790,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1047790/?format=api",
"text_counter": 351,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "baadaye akawa Mkuu wa Mkoa. Ninakumbuka alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo makao makuu yalikuwa Mji wa Mombasa. Sen. Haji alikuwa mnyenyekevu sana. Ungemwona katika shughuli zake, hungedhani alikuwa mtu mwenye mamlaka makubwa na kwamba alikuwa amefanya kazi kubwa katika Serikali ya Kenya. Binafsi, niliwahi kuswali naye Swala ya Alfajiri katika msikiti karibu na nyumbani kwake, Westlands. Alikuwa anakuja msikitini alfajiri peke yake hata bila mlinzi. Inamaanisha kwamba hakuwa na hofu kwa lolote ambalo lingemfika huku akiwa na umri wa karibu miaka 80. Hakuwa na uoga kwamba jambo lolote lingempata wakati huo wa alfajiri. Bw. Spiaka wa Muda, pia akija Mombasa kwa shughuli zake za kikazi ama kujivinjari, alikuwa na mpango wa matembezi katika ufuo wa bahari asubuhi. Watu wengi hufanya mazoezi kule asubuhi na yeye alikuwa akijiunga nao kutembea kilomita saba hadi 10 hivi kwa siku, ili kuweka mwili wake katika hali nzuri ya kiafya. Alikuwa akitembea bila mlinzi na hata bila hofu kwamba jambo lolote lingemfika mahali kama pale. Kwa hivyo, kitu ambacho tunasoma katika maisha ya Sen. Haji ni kwamba, alikuwa mnyenyekevu, mpole na mtu wa kauli dhabiti. Ulikuwa huwezi kumwondoa katika msimamo aliochukua bila sababu nzuri za kimsingi. Tulifurahia sana wakati tulipokuwa tunapambana na mambo ya ugavi wa rasilimali mwaka jana, tukiwa na Sen. Haji kama mzee wetu katika kikundi kile. Kwa hakika, uongozi wake ulionekana kwamba ni mtu mwenye kauli dhabiti na hakuwa mtu wa maneno mengi. Ijapokuwa alikuwa anapinga upande wa Serikali kuhusiana na swala hili la ugavi wa rasilimali, hakutoa maneno ya kukejeli wala machafu ya kuudhi ule upande mwingine. Bw. Spika wa Muda, Sen. Haji alikuwa mpole, mnyenyekevu na alihudumia nchi hii bila ya kutaka mengi. Angekuwa mtu wa kutaka mengi, angekuwa alipata mengi kabisa kutoka kwa Serikali, kutokana na nafasi aliyokuwa nayo kibinafsi. Huwezi kusikia kuwa Sen. Haji alikuwa na kashfa ya aina yoyote. Ndio maana alipochaguliwa kuongoza BBI, hakuna aliyepinga uteuzi wake na alifanya kazi kulingana na vile alipewa afanye na mwenzake, Sen. Wako. Wakati tunaomboleza kifo chake, lazima tukubali pia katika ulimwengu, tuko kwa muda maalum, ambao Mwenyezi Mungu mwenyewe ametuwekea. Tutakapoondoka, lazima tuwache sifa nzuri kwa wale watakaotufuata. Waisilamu, Mwenyezi Mungu anatuambia katika Kitabu chetu takatifu kwamba, kila nafsi itaonja mauti. Kwa hivyo, mwenzetu yake ilikuwa jana, sisi twaomba Mwenyezi Mungu aweke roho yake mahali pema peponi. Sisi tuliyobaki, tuige mfano wake ili tuishi maisha mazuri hapa duniani na kesho ahera tutakapokuwa kwa Mwenyezi Mungu."
}