GET /api/v0.1/hansard/entries/1048015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1048015,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048015/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Gilgil, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Martha Wangari",
    "speaker": {
        "id": 13123,
        "legal_name": "Martha Wangari",
        "slug": "martha-wangari"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Naungana na wenzangu kutoa rambirambi zangu binafsi, za familia yangu na za watu wa Gilgil kwa familia za wendazao. Hili Bunge la 12 tumekuwa na misiba mingi sana ambayo inagusa wenzetu na tunaomba kwamba Mola aisitishe na isipite hapo. Tunaomba pia Mungu awalaze mahali pema. Niliweza kutumikia na Seneta Yusuf Haji kwenye Bunge la 11 kama Seneta na alikuwa mwenye heshima kwa wazee na wadogo zake. Alikuwa mwenye uadilifu, mwenye maarifa na nafikiri pia aliweza kutudhihirishia kwamba unaweza kuingia Bunge kwa kuteuliwa na ukarudi pia ukaomba nafasi kwa kuchaguliwa. Alichaguliwa sio mara moja, sio mara mbili bali karibu miaka 20. Kwa hivyo, ametutengenezea njia na sisi sote tunamfuata na tunasema kwamba hata wakati Raisi alimchagua kuwa kiongozi katika huu mchakato wa kuleta uwiano, alikuwa ameangalia uadilifu wake wa kazi. Alikuwa mcha Mungu na alipenda watu wote bila kuangalia kabila wala miaka. Mhe. Spika, hata tunapoandika kitabu cha historia cha nchi hii, marehemu Mhe. Yusuf Haji atakuwa amejiandikia sio aya bali sura nzima kwa sababu ya kazi yake. Asante, Mhe. Spika, kwa nafasi hiyo."
}