GET /api/v0.1/hansard/entries/1048043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1048043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048043/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": " Asante, Mh. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nitoe pole zangu na pole za Kaunti ya Samburu kwa wenzetu ambao wameaga dunia. Seneta Yusuf Haji alikuwa kiongozi ambaye hatasahaulika nchini Kenya. Seneta Haji ni mtu ambaye aliishikilia Kenya. Tangu utotoni mwake, alihudumia umma enzi za marais wanne wa Kenya. Ni mzee ambaye tunasema, kwa sababu ni Mwenyezi Mungu amemchukua, amuweke mahali pazuri kwenye roho yake. Seneta Haji ni mtu ambaye aliwalea wengine wetu; ni mzee ametulea. Ni mzee aliyejua njia ya kuongoza. Yeye ni mmoja wa watu ambao walitufanya sisi kuwa viongozi. Seneta Haji hatasahaulika. Mwenyezi Mungu ndiye atakayeturudishia mtu mwingine katika nafasi yake mwenye atakuwa kama yeye. Yeye ni mzee ambaye hakuwa na ubaguzi, hakuwa na ukabila, hakuwa na chochote. Alikuwa mtu ambaye akikwambia “ndiyo” inakuwa “ndiyo” na akikwambia “hapana” inakuwa “hapana.” Nashukuru kwa sababu wakati alipokuwa mwenyekiti wa BBI, Seneta Haji hakuwa mtu aliyetaka mambo ya kwenda hivihivi. Ni mzee aliyekuwa anasimama kama kiongozi. Alikuwa anatuambia kwamba hakuna chochote kitawekwa kwenye BBI isipokuwa ni kile mwananchi…"
}