GET /api/v0.1/hansard/entries/1048070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1048070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048070/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana Bw. Spika. Kwanza, kwa niaba yangu na ile ya Wanamvita, ningependa kutoa pole kwa familia na jamii ya Mhe. Oroo Oyioka ambaye alikuwa Mbunge wa Bonchari na ile ya Marehemu Mohamed Yusuf Haji ambaye alikuwa Seneta wetu. Kibinafsi, ningependa kutoa pole zangu kwa wanawe Abdul na Noordin. Bw. Spika, mengi yameweza kuzungumzwa katika Jumba hili lakini kuna mafunzo ambayo vifo hivi vinafaa kutufunza sisi. Kwanza, hamna ambaye ana mkataba na Mwenyezi Mungu ni lini ataenda mbele ya haki. Haya mambo ya watu kujigamba kuhusu 2022… Ikiwa kuna lolote mwanasiasa anapaswa kujifunza na vifo hivi ni kuwa yeyote anaweza kwenda mbele ya haki wakati wowote. Pili, mkumbuke leo tunazungumzia wenzetu walioenda mbele ya haki. Kesho mimi na mmoja yeyote atakayekuwa hapa na wengine wote watakaokuwa hapa, wataenda mbele ya haki. Swali ni: Tutakumbukwa na yapi ambayo tuliweza kuwatendea watu wetu? Tusiwe ni wenye kujigamba lakini tujue yakuwa binadamu akienda mbele ya haki hukumbukwa kwa yale aliyoweza kuyafanya. Mwishowe, katika dini ya Uisilamu, hamna aliye na hadhi zaidi ama aliye na fedha zaidi ama mwenye kujulikana zaidi. Unafariki alfajiri, ikifika adhuhuri ama alasiri, uko chini ya mchanga."
}