GET /api/v0.1/hansard/entries/1048114/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1048114,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048114/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "mashujaa wetu watatu ambao walituacha. Nikizungumzia Mhe. Nyachae na Sen. Haji, hawa ni viongozi ambao wametoa michango kubwa katika Taifa la Kenya haswa katika nyanja za maendeleo. Nikizungumzia Sen. Haji, si kwamba ni Garissa peke yake imepoteza kiongozi, lakini ni Kenya kwa jumla haswa jamii ya Kiislamu. Sen. Haji alikuwa kama kielelezo chetu. Alikuwa kama jicho letu kama jamii ya Kiislamu tukimuangalia sana katika nyanja za maendeleo. Tumeona sifa zake za kutokuwa na dosari katika uongozi wake. Pia ameonyesha njia ya kuunganisha jamii kule Kaskazini-Mashariki wakati jamii za watu wa sehemu hizo walikuwa wakizozana na kuweza kuwapatanisha. Haya yote ni kuonyesha kuwa ni mtu ambaye hakuwa na ubinafsi. Alikuwa mtu wa ukweli, shupavu na kusimama na jambo la kutetea jamii na Kenya kwa jumla. Kwa hivyo, sisi kama Taifa, tumepoteza kiongozi ambaye sasa angekuwa mstari wa mbele kuongoza lile jopo la BBI. Katika kumpa tuzo, tutapitisha mswada wa BBI na pale alipo, atajua kwamba Wakenya walisimama naye katika kuleta Wakenya pamoja tuwe taifa moja na kushirikiana katika kuleta nyanja za maendeleo. Sisi Waislamu pia tunasema: “ Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un .” Yaani tulitoka kwa mwenyezi Mungu, na kwa mwenyezi Mungu ni marejeo."
}