GET /api/v0.1/hansard/entries/1048251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1048251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048251/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika. Kupitia Kanuni ya Kudumu Nambari 44 (2) (c), naitisha jawabu kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama kuhusu upigaji risasi uliosababisha kuumia kwa Bw. Sadat Salim Abdallah mwenye umri wa miaka 42, Bw. Fahal Salim Abdallah mwenye umri wa miaka 35 na kuuawa kwa Amur Ahmed Salim, kijana mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 24, risasi zilipomiminwa kwenye miili yao. Alhamisi iliyopita, tarehe 11, Sadat, Fahal na Amur walipigwa risasi kadhaa na watu wanaosemekana kuwa polisi katika hali isiyoeleweka. Walikuwa nje ya duka dogo la M-PESA eneo la Kaloleni, Mvita. Yaliyotokea ni kifo cha Amur na majeraha makubwa kwa Fahad na Sadat. Mhe. Spika, la kushangaza, kusikitisha na kutia wasiwasi zaidi ni kuwa polisi hawajafanya uchunguzi wowote hadi leo. Hawajarudi kwenye eneo ambako uhalifu huo ulitokea. Hawajaongea na majirani ama watu ambao waliona tukio hilo, wala hawajaitisha rekodi za CCTV katika maeneo ya karibu mahali pale. Juzi nikiwa hospitali, nilithibitisha kuwa polisi hawajawafuatilia wale walioumizwa ili kuweza kuchukua kauli zao. Nimeongea na familia ya marehemu na hadi leo, hawajajulishwa chochote wala kuambiwa waende waandike maelezo yoyote. Mhe. Spika, kupitia haya, twastahili jawabu kupita kwa Mwenyekiti wa Usalama kuhusu mambo matatu yafuatayo: (i) Serikali imeweka mikakati gani kuhakikisha kwamba uchunguzi unafanywa ili wale waliosababisha madhara na kifo wapelekwe mbele ya haki? (ii) Ni mikakati gani Serikali inaweka kuhakikisha kwamba familia za walioathirika kwenye mkasa huu wamepewa fidia ikiwemo kulipa malipo ya hospitali, na ni lini jambo hili litaweza kufanyika na kumalizika? (iii) Serikali ni lazima iwe wazi na kutuelezea imeweka mikakati gani kuhakikisha kwamba kuna hali ya usalama, haswa wakati huu tulioko wa dijitali. Wameweka mikakati gani ili mambo kama haya yakitokea tuweze kujua bila ya kuchelewa wahalifu ni akina nani? Ahsante, Mhe. Spika."
}