GET /api/v0.1/hansard/entries/1048304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1048304,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048304/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms.) Ruweida Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Lamu (CWR), JP): Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia. Mwanzo, ningependa kushukuru Kamati. Kamati hii ya Mazingira ni Kamati ya ungwana sana. Sisi, watu wa Lamu, tunaitambua hii kamati zaidi kushinda kamati nyingine yoyote. Tulifanya petition, wakaenda Members wote mpaka Ndao, wakaona hali ilivyo, wakatusaidia na hiyo iko kwenye records . Kwa hivyo, pongezi sana Kamati. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Repoti hii. Katika pointi walizotoa, ya kwanza nikinukuu, wamesema: “Misitu yetu na hifadhi za wanyama ni muhimu kuzihifadhi.” Hizi ndizo rasilimali zetu. Lakini wakati tunazihifadhi, tufikirie Kenya yote pia. Pahali kama Lamu kuna Dodori National Reserve ambayo inaweza kuleta pesa nyingi sana hapa nchini. Lamu kuna mambo mazuri lakini yamenyamaziwa, hayaangaliwi. Hivyo basi, pesa zinapotea bure na hatupati hizo pesa. Kuna simba pale Dodori National Reserve ambao huvua samaki. Ni kitu ambacho hakitokei sehemu zingine. Hii ingekuwa kama ule uhamiaji wa nyumbu kule Maasai Mara ambayo ingetusaidia kuleta watalii. Kwa hivyo, mkiangalia misitu hii, muangalie pia Dodori National Reserve. Jambo la pili amezungumzia ni vita kati ya wanyama na binadamu. Vita hivi viko katika kila kaunti, lakini Kaunti ya Lamu zaidi. Kwa mfano, kuna watu wa Mkokoni ambao wanalima na hawasaidiwi na matrakta. Wanalima kwa nguvu zao lakini kabla hawajavuna, nyati huenda kuvuna. Kisha, wao hukaa kwa muda bila kulipwa au pengine hawalipwi kabisa. Jambo hilo huwafanya wafe moyo. Kuna sehemu mbali mbali zingine kama kule mainland ambapo wamekufa moyo maanake wanaathiriwa na wanyama na hawalipwi. Amezungumzia pia udhibitisho wa haki kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo yako karibu na wanyama hao. Kusema ukweli, wakianza kwenda muundo huu, watasaidia sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}