GET /api/v0.1/hansard/entries/1048305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1048305,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048305/?format=api",
"text_counter": 360,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms.) Ruweida Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kuna wanyama ambao ni hatari na huleta shida kwa wananchi. Kule Maasai Mara, wameona kwamba simba ni muhimu kwao na wasimuue kwa sababu analeta rasilimali. Sisi Lamu hatujaona umuhimu wa mnyama. Wale wanyama ambao twapenda kuwala kama chakula, kwa mfano kasa, Serikali haitaki waliwe. Kule Lamu kwa Wabajuni, kasa ni chakula cha kitamaduni. Inajulikana kwamba mnyama huyu ni mtamu ukimla na ni dawa pia. Lakini kwa sababu ya kuchunga mazingira, tunakatazwa kumla na sheria kali zimewekwa kuwa utafungwa miaka 25. Serikali haijakuja na mbinu za kutuonyesha tumuhifadhi mnyama huyo kivipi. Kama tumekatazwa kumla, basi atusaidie tupate manufaa kama vile watu wa Maasai Mara wanavyopata. Lau Kamati hii itafuata hayo yaliyozungumziwa, basi sote tutajihisi kuwa Wakenya."
}