GET /api/v0.1/hansard/entries/1048408/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1048408,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048408/?format=api",
"text_counter": 64,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kujiunga na Maseneta wenzangu kuunga mkono Taarifa iliyoombwa na Seneta wa Makueni. Ni kweli kwamba Serikali inajaribu kulinda Shirika la Ndege la Kenya Airways kwa sababu hata Mombasa wamezuia mashirika mengine ya kuweza kusafirisha abiria kutoka nje. Wakati umefika sasa kuona kwamba Wakenya tunapata value for money ; hatuwezi kuwa tunaendelea ku subsidize ama kuitilia nguvu Kenya Airways wakati wao wenyewe wana uzembe na utepetevu katika kuendesha kazi zao. Tunaomba kwamba Kamati husika iingilie swala hili kwa undani zaidi kuhakikisha kwamba kama kuna jambo lolote ambalo linaweza kufanyika kuongeza idadi ya ndege zinazokuja kutoka UAE, ziweze kupatikana kwa sababu hii itasaidia Wakenya wengi ambao wanasafiri kibiashara na vile vile kikazi katika nchi hizo za Uarabuni. Asante sana, Mhe. Spika."
}