GET /api/v0.1/hansard/entries/1048710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1048710,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048710/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia malalamiko ambayo yameletwa na Sen. (Dr.) Mbito. Ninampongeza Sen. (Dr.) Mbito na shule hiyo ya Kitale kwa kuamua kuleta malalamiko haya katika Seneti. Malalamiko yaliyoletwa yanaonyesha vile ulaghai na ukosefu wa maadaili umewakumba baadhi ya viongozi katika Jamhuri yetu ya Kenya. Haiwezekani kwamba mtu aliyechaguliwa kama mlezi wa shule awe wa kwanza kuchukua ardhi ya shule kwa maslahi ya kibinafsi. Huo ni ukosefu was maadili. Ni lazima Bunge la Seneti ikemee suala kama hilo. Hii siyo kesi pekee, kuna kesi nyingi kama hizi. Kuna shule nyingi ambazo ardhi zao zilinyakuliwa wakati wa nyuma katika hali kama hizi ambapo waliokuwa wakinyakua walikuwa labda ni viongozi kama madiwani, wabunge na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali ya Serikali. Ni jambo ambalo tunafaa kukemea sana kama Bunge. Pia, jambo la kusikitisha ni kwamba kwa muda wa zaidi ya miaka kumi sasa, tumekuwa na Tume ya Ardhi (NLC) ambayo hii ni baadhi ya kazi ambazo walikuwa wanatakikana kufanya ili zile ardhi zote za umma zilizokuwa zimeibiwa ziweze kurejeshwa. Nina imani kwamba Kamati ya Ardhi na Mali ya Asili ikiongozwa na Sen. Mwangi, itasimama kidete kuhakikisha kwamba ardhi hii inarudi kwa ile shule ya Msingi ya Kitale. Ni zaidi ya miaka 80 tangu walipopewa ardhi ile. Shule ile ikiwa itapanuka mpaka iwe na sekondari na chuo kikuu, itakuwa ni jambo ambalo litasaidia kuinua elimu katika eneo la Kitale na nchi yetu kwa jumla."
}