GET /api/v0.1/hansard/entries/1048783/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1048783,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1048783/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kusema ukweli, matatizo ya madiwani waliohudumu yanasikitisha kwa sababu Bunge lilipitisha kwamba walipwe marupurupu ya kiinua mgongo, lakini mpaka sasa hawajalipwa. Nikizungumzia Mombasa, mwaka uliopita tuliwapoteza madiwani wanne wa zamani, wakiongozwa na Mheshimiwa Shekhu ambaye alikuwa Meya wa Mombasa, Mheshimiwa Juma Goshi aliyekuwa Naibu wa Meya, Mheshimiwa Seidh Mathias na Mheshimiwa Mwakunyapa. Wote hao waliaga wakisubiri pesa hizi ili ziweze kuwasaidia katika maisha yao. Bw. Spika, nina madiwani wengine wawili ambao walistaafu na wako vitandani hivi sasa. Hawana pension yoyote na wanapata shida ya pesa za matibabu. Kuongezea pia ni kuwa pesa za wale ambao walihudumu katika East African Community hawajalipwa. Nchi zingine kama Uganda na Tanzania wameweza kuwalipa wafanyakazi ambao wamestaafu katika East African Community. Bw. Spika, Kamati husika ni lazima iingilie jambo ili kwa undani zaidi ili tujue ni kwa nini maazimio ya Bunge hili hayawezi kutekelezwa. Asante, Bw. Spika."
}