GET /api/v0.1/hansard/entries/1049124/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1049124,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049124/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kutumia fursa hii kumpongeza Mhe. Kassim Tandaza kwa kuja na Mswada huu. Sote tunafahamu kwamba ukulima ndio uti wa mgongo katika maisha ya leo. Mmea huu, ambao Mhe. Kassim Tandaza ameutaja, ni mmea ambao unapatikana katika sehemu za Pwani, hususan katika maeneo ya Lamu na Kwale. Kabla sijazungumzia mmea huu, ningependa kuzungumzia swala nzima la ukulima na faida ya ukulima, hususan katika nchi hii na eneo la Pwani. Mbali na kuwa tunafahamu kwamba ukulima ndio muhimu sana katika uchumi wetu, tumeona wazi ya kwamba watu wanategemea ukulima katika mambo mengi. Kwa masikitiko makubwa, nikizungumzia eneo la Pwani, ukulima umefifia sana kwa sababu ya kutotiliwa nguvu na kutosaidiwa na Serikali. Ninaamini kwamba Wapwani wanapenda maswala ya ukulima na wanajitahidi sana. Lakini katika swala hili, Wapwani hawajasaidika na namna ya kujiendeleza na ukulima wao. Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, tunapojadili swala hili, ni vyema tufahamu na Serikali ijue ya kwamba Wapwani wanahitaji usaidizi katika kuendeleza ukulima. Kuwe kwamba tuko na ardhi za kutosha na mimea ya kutosha. Katika hali hii, tunaamini ya kwamba angalau tutapata misaada kama vile misaada mingine inavyotolewa katika sehemu nyingine katika nchi hii. Tukifanya hivyo, Pwani itakuwa na ukulima mwingi na wengi watajiingiza katika jambo hili ili waweze kusaidika na kusaidiwa kuliendeleza jambo hili. Vile clienteles, ni vyema tufahamu kwamba katika hali ya uchumi wetu hivi sasa, ukulima ndio jambo ambalo tunahitaji kulipea kipaumbele. Ardhi tuko nazo na wanaohitaji kufanya ukulima tuko nao lakini Serikali lazima ijitokeze, kupitia kwa wizara husika, kuhakikisha ya kwamba wakulima hawa wamesaidiwa kwa njia zote wanazotaka na kuhamasishwa, ili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}