GET /api/v0.1/hansard/entries/1049199/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1049199,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049199/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": {
        "id": 13357,
        "legal_name": "Paul Kahindi Katana",
        "slug": "paul-kahindi-katana-2"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza nataka kumpongeza Mjumbe wa Matuga, Mhe. Kassim Tandaza kwa kuleta Mswada huu wa mabdiliko. Wakati umefika sasa wa Wizara ya Kilimo kufanya utafiti kwa kila mmea katika majimbo yetu ili wajue ni mmea upi waweza kutumika kuzalisha na kuleta mapatao katika maeneo haya na nchi kwa jumla. Kwa muda mrefu, mimea kama kahawa, chai, korosho, na mnazi zilikuwa zikisifika kwa mazao yao. Lakini, kwa sasa mimea hizi zimefifia. Tunajua kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii. Serikali inatakikana kuweka bajeti kubwa kwa Wizara ya Kilimo ili utafiti ufanywe wa kusaidia wakulima wa mimea hizi. Kule pwani, tuko na mimea ya mnazi mkorosho na Bixa. Mimea hii imekua ikileta mapato lakini, tangu viwanda vya mkorosho na Bixa vifungwe, hali ya uchumi wa jimbo la pwani imerudi nyuma. Ni jambo la aibu kuwa kwa sasa tunaagiza tui la nazi kutoka nchi ya Malaysia ilihali pwani tuna mmea huu ambao unaweza kutumika kutoa zao hilo. Vile vile, kama Serikali inaweza kufanya utafiti, wa mimea hii mitatu pwani, inaweza kutoa suluhu la ukosefu wa ajiri katika jimbo la pwani na kenya nzima. Kwa muda mrefu, ifikapo wakati wa uchaguzi, watu wengi huja pwani na kuwahadaa wapwani kwamba watawekeza kwa mnazi na kufufua viwanda vya mkorosho na Bixa lakini, ukienda kule baada ya uchaguzi, mimea hii haitambuliki. Nataka kuunga mkono Mswada huu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}