GET /api/v0.1/hansard/entries/1049200/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1049200,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049200/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": {
        "id": 13357,
        "legal_name": "Paul Kahindi Katana",
        "slug": "paul-kahindi-katana-2"
    },
    "content": "Bixa, Mkorosho na nazi ziletwe kataika ibara ya kwanza ya mimea ambayo inaweza kutumika kuzalisha na kuleta mapato katika taifa letu. Mnazi peke yake unaweza kuajiri zaidi ya watu alfu kumi. Kwa muda mrefu, watu wamekuwa wakiongea kuhusu bidhaa moja ya mnazi ambayo ni pome peke yake. Mnazi una Zaidi ya bidhaa kumi na mopja. Kwa mfano, fuvu la nazi linaweza kutumika kutengeneza vifungo. Kwa sababu kilimo kimegatuliwa, serikali za kaunti zinaweza kuleta mitambo na kuajiri vijana wengi, ili waweze kujikimu kuliko kuwapa maslasha wafyeke na kusafisha mitaro ya maji-taka. Pesa zinazotumika kule zinaweza kutumika kuwekeza kwa kilimo. Mhe. Naibu Spika, kama waweza kukumbuka, mti wa mnazi katika nchi ya Malaysia umefanya nchi hiyo kukua kiuchumi. Serikali haijafanya utafiti muhimu wa kuhakikisha kwamba mti huu unaweza kutupatia pato. Wakati huu wa ugonjwa wa COVID-19, ni kilimo peke yake abayo imeweza kusaidia wananchi kujikimu kimaisha. Naunga mkono Bixa kuletwa kwa ibara ya kwanza ya mimea. Vile vile, mnazi na korosho ziwekwe katika ibara ya kwanza ili tupate pesa ya kufanya utafiti na kutafuta masoko nchini na nchi za kigeni. Naunga mkono Mswada huu wa mabadiliko. Ahsante."
}