GET /api/v0.1/hansard/entries/1049202/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1049202,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049202/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hi. Mimi pia najiunga na wenzangu kumpongeza ndugu yetu mhe. Tandaza, mbunge wa Matuga kwa kuleta Mswada huu ambao unarekebisha sharia za mimea hapa nchini. Kwanza, ningepende kuto risala zangu za rambi rambi kutoka kwangu pamoja na jamii yangu, eneo bunge la Taveta na Taita Taveta kwa ujumla kwa jamii za wabunge waliokufa. Bunge hili la kumi na mbili limepata kipigo cha kuwapoteza wabunge wengi. Tunawaombea na tunajua wametutangulia mbele ya haki. Kule walikokwenda, Mwenyezi Mungu aweke roho zao pahali pema peponi. Mti huu wa Bixa au mrangi kama unavyoitwa pwani ni mti muhimu sana. Mbegu zake ni za muhimu. Si bure tu Mhe. Tandaza amelivalia njuga jambo hili. Eneo lake haswa kule kwale ndiko kiwanda cha Bixa kiliko ambacho inaweza kuhakikisha mmea huu wa Bixa unapatia watu faida. Ni sawa ikiwa mmea huu wa Bixa utaorodheshwa pamoja na mimea mingine muhimu hapa nchini. Si jambo la kutosha kuorodhesha tu. Orodha hizi zikitoka, mimea hii lazima ipatiwe kipaumbele. Serikali ya taifa na serikali za magatuzi ziangalie kuwa mimea hii inapatiwa umuhimu haswa kwa kuwasaidia wakulima waweze kupata mbegu zinazofaa na kuwafunza ukulima wa kisasa maana yake, kule mashinani zaidi wakulima wengine hulima kiholela kwa sababu hawapatiwi mwelekeo wa njia za kulima za kisasa, ili wapate haki yao kutokana na jasho lao la ukulima. Maeneo mengi yana mimea tofauti tofauti ambayo yana faida hapa nchini. Kwa mfano, kuna mkorosho, mnazi, ndizi kutoka maeneo yetu ya Taveta na maeneo mengi hapa nchini, vile vile mihogo, viazi vitamu, ndegu iliyotajwa kuwa inapandwa hapa nchini na mimea mingine mingi ikiwemo kahawa na chai. Si siri kuwa vitu vyote vinavyopandwa hapa nchini ni vya umuhimu na vinatumika ulimwengu mzima isipokuwa wakulima wasipopatiwa ujuzi wa kuhakikisha kuwa wanaweza kulima kwa njia za kisasa na kuhakikisha mavuno yao yanakuwa ya gredi ya juu, itakuwa shida kwa mkulima kupata haki ya jasho lake alilolitoa. Ukweli ni kwamba, hapa nchini mambo ya kilimo ni ya muhimu. Yamewezesha wazazi kujiendeleza na kusomesha watoto na kubadilisha uchumi wa nchi hii. Lakini hivi juzi tuliona kuna vitu ambavyo vinaweza kukaa sana na kuna ile The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}