GET /api/v0.1/hansard/entries/1049203/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1049203,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049203/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "mimea ambayo mazao yake hayawezi kukaa kwa muda mrefu. Kwa mfano, nataka kuzungumzia ndizi ambazo zinatoka kule kwetu. Utakuta kuwa ndizi hazikai kwa muda mrefu. Ni kati ya ile mimea ambayo tunajua itakuwa na matatizo. Tunajua mahindi yanaweza kukaa kwa muda lakini juu ya hiyo, mahindi pia lazima yapatiwe bei inayostahili. Vilevile, Serikali inafaa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa taaluma ya kilimo wanaweza kuwasaidia wakulima kupata haki yao. Ukienda nchi za nje, utakuta kuwa kahawa na chai nzuri zaidi zinazotumika kule ni zile za kutoka Kenya. Saa zingine wanachanganya kahawa yetu na zingine, lakini zaidi sana kahawa ya Kenya inasifika kila mahali. Ukienda Marekani, utakuta ndiyo inasifika; kila mahali duniani. Vilevile, wamechukua chai yetu wakachanganya na chai zingine ambazo hazina utamu kama ya Kenya. Chai yetu inajulikana ulimwengu mzima. Swali ni kuwa, je wakulima wetu wanapata haki yao? Hilo ndilo swali kubwa ambalo Serikali yetu itatusaidie ili wakulima wetu wapate haki yao, sio eti wale wanaofanya biashara ya mimea hii na mavuno haya ya kahawa ndio wanaofaidika peke yao. Bixa, ama mrangi, ni mbegu zinazotumika kutengeneza rangi na hata kwenye chakula na kwa vitu vya urembo vya akina mama. Juu ya hapo, kitu ambacho kinaweza kutumika kwenye chakula ni kitu ambacho Serikali ingekipatia nguvu sana ili kiwanda kile kijengwe upya ili wakulima wa maeneo hayo na hata wakulima wengine wahimizwe kulima na kuvuna mbegu za mrangi. Ni dhahiri kuwa Kenya tumezoea kufanya ukulima wa kutegemea mvua. Mvua ikichelewa tu kidogo, basi kumeharibikiwa kwote. Serikali kuu imekuwa ikiweka mkazo kuhakikisha kuwa imejenga madimbwi ya maji kila mahali. Lakini naona kuwa ugawaji wa hayo madimbwi hauendi inavyotakikana. Hivyo basi, kuna umuhimu wa Serikali kuhakikisha kuwa madimbwi hayo ya maji yanatengenezwa kila maeneo ili wakulima wote, hata wenye kutoka maeneo kame, waweze kupata maji. Mvua ikinyesha tunapata mafuriko ambayo yanaharibu kila kitu - yanaua watu na mifugo na kumaliza mimea. Maji haya yakitumika vizuri yataweza kutuletea faida wakati wa ukame. Namalizia kwa kumuunga mkono na kumpongeza kaka yangu Mhe. Tandaza kwa kuleta Mswada huu ambao utarekebisha orodha ya mimea ambayo imetejwa kwenye sheria ya mimea hapa nchini. Naunga mkono."
}