GET /api/v0.1/hansard/entries/1049216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1049216,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049216/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mbogo Ali (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kisauni, WDM-K): Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu. Nataka nimshukuru Mheshimiwa Tandaza Sawa, Mjumbe wa Matuga, kwa kuuleta Mswada huu Bungeni uweze kujadiliwa ili mumea wa mrangi au Bixa uweze kutambulika na kuwepo kwenye ratiba ya mimea bora kama mimea mingine muhimu katika Jamhuri ya Kenya. Mrangi au Bixa ni mumea muhimu sana kwa watu wa Pwani. Mumea huu unafanya vizuri sana katika maeneo ya Lamu na Kwale, na haswa katika Eneo Bunge la Mheshimiwa Tandaza, Tiwi. Pwani nzima, kuna eneo la Kwale ambako tuko na kiwanda kidogo cha kibinafsi kinachotumika kuongeza thamani ya mumea huu. Kiwanda kile kimekosa ufadhili. Pia, kiwanda hicho kimekosa faida kutoka kwa mumea huo ili kiweze kukua. Hivi juzi, katika maeneo ya Lamu, tuliona wakulima wa mrangi barabarani wakiandamana kwa sababu ya kukosa soko la mazao yao. Ukiangalia, mtu anatoke maeneo ya Lamu katika eneo la Mpeketoni, anabeba mazao yake karibu kilomita mia sita mpaka Tiwi ndio apate kile kiwanda kidogo ili aweze kuuza mazao yake. Hiyo ni haki kweli? Tukikumbuka kule nyuma, shirika la ndege nchini, Kenya Airways, lilikuwa likiyumbayumba bila kupata faida. Serikali Kuu iliingilia kati na kulipa shirika hilo mgao wa fedha ili lisizame. Kiwanda kile ni cha kibinafsi na kwa hivyo tunaomba Serikali Kuu pia iweze kukiangalia ili kisizame ila kiinuke na kuwa kiwanda cha kileo ili kiweze kufanya kazi kubwa na kutoa ajira nyingi kwa watu wa Pwani, na hususan watu wa Tiwi na Kwale kwa jumla. Mrangi, kama tulivyosikia kutoka kwa watangulizi, ni mumea unaostahimili jua, magonjwa na unafanya vizuri sana katika sehemu yenye joto kama vile Pwani. Kabla ya teknolojia kuimarika, akina mama kule Pwani walikuwa wakitumia mrangi kama kipodozi mbadala cha"
}